2 Julai 2025 - 13:21
Source: Parstoday
Araqchi: Kurutubisha madini ya urani ni mstari wetu mwekundu; katu hatutalegeza kamba

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, teknolojia na sayansi ya kurutubisha madini ya urani haiwezi kuharibiwa kwa mashambulizi ya mabomu.

Sayyid Abbas Araqchi, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema hayo katika mahojiano aliyofanyiwa na Kanali ya Televisheni ya CBS na kubainisha kwamba,  inawezekana kushambulia vituo vya nyuklia, lakini teknolojia na sayansi ya kurutubisha haiwezi kuangamizwa kwa mashambulizi ya mabomu.

Waziri Araqchi amesema bayana kwamba, mpango wa amani wa nyuklia wa nchi yetu umekuwa ni fahari na heshima ya taifa.

Araghchi aliongeza: "Tumepitisha siku 12 za vita vya kulazimishwa, hivyo watu wa taifa hili hawataacha kwa urahisi urutubishaji madini ya urani."

Pia aliongeza: "Wakati wa vita, tumeonyesha na kuthibitisha uwezo wetu wa kujilinda, na ikiwa tutashambuliwa kwa njia yoyote, tutaendelea kufanya hivyo."

Katika mahojiano yake hayo na CBS, Araghchi alisema: "Ili kuamua kufanya mazungumzo upya, lazima kwanza tuhakikishe kwamba Washington haitarudi kutulenga na mashambulizi ya kijeshi wakati wa mazungumzo."

Kadhalika Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran ameeleza kwamba,: "Sidhani kama mazungumzo yataanza tena kwa haraka kiasi hicho. Pamoja na mambo haya yote, bado tunahitaji muda zaidi na milango ya diplomasia kamwe haitafungwa."

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha